Alitoka nchini mwishoni mwa mwezi wa Januari akielekea Denmark ambako alikua amealikwa katika sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya legendari wa mziki wa reggae marehemu BOB MARLEY. Kando na sherehe hio, Nyota alikua alikua atakita kambi kwa miezi miwili na usu nchini Denmark ambako alikua anafanya tour na kufanya collabo za wasanii wakimataifa. Baada ya kukamilisha tour yake wiki jana, alirudi nyumbani na akafanya show Skylounge, show ambayo ilijaaa sana na kuhudhuriwa na watu wengi maaruf na mashabiki wengi sana. Hapo jana, siku ya Jumatatu, Susumila na Producer Amz waliandaa sherehe ya kumkaribisha rasmi Nyota Ndogo . Sherehe hio ambayo iliitwa PWEZA PARTY iliweza kuhudhuriwa na familia ya Nyota Ndogo, wasanii kama vile Ali B, Pero, CashEra, Hustla Jay, Vivonce, Wazo Baba, Res T, Gaspery, Msanii Jrg na wenginene wengi. marafiki na washika dau wengine katika tasnia ya burudani kama vile mtangazaji Lukas De Mackinon wa FM, Producer Jay Crack, Hassan Faisal, Kibibi ...