Posts

Showing posts from June, 2016

Lizz Jahsolja Apata Shavu Katika Kedia Awards

Image
Lizz Jahsolja ambaye ni mmoja wa finalists katika kitengo cha Model Of The Year, Kedia Awards 2016 amepata bonge  la shavu katika tuzo hizo. Lizz ambaye amekua akipeperusha bendera ya pwani katika tuzo hizo ambazo zimepangwa kufanyika mwezi wa Oktober ameweza kujiondoa kama muwaniaji wa tuzo baada ya kupeqa shavu na kufanywa administrator. "Katika position yangu mpya nitakua na jukumu la kuchangua na kuandaa wasanii ambao watakua wanatumbuiza katika tuzo hizo." Lizz ameonyesha kujawa na furaha ameeleza meza yetu ya habari.  Japo amekatakaa kufunguka kwa kina kuhusu benenfits atakazopata kama administrator Lizz ameeleza kwa kifupi tu kwa kusema "its worth it"

Uja Uzito Ndio Ulimnyamazisha Shiney Katika Mziki

Image
Msanii kutoka studio za Big Foot, Shiney ambaye pia ni 'babymama'  na pia mpenzi wa Producer Baindo amefunguka na kusema kuwa kimya chake katika mziki kimesababishwa pakubwa na ujauzito aliokua nao. Kulingana na Shiney ni kwamba baada ya kuachilia track ya Kidonda Cha Mapenzi, ratiba yake ilikua ni kut ayarisha video tatu mfululizo ambazo mashabiki wake wamekua wakizililia lakini kabla ya kuanza project hizo baraka za ujauzito zikamfikia. "Mimi sio msanii wa kwanza kujifungua kwa hivyo kujifungua kwangu hakutawahi kuathiri kabisa kazi yangu ya mziki.....Kuna ngoma ambayo nimefanya na Mr Bado ambayo nimeifanya saa hii nasubiri kurudi sawa alafu kazi iendelee. Baada ya hapo ndio nitaanza kushughulikia video ya Jicho maana hiyo ndio mashabiki wangu wana demand" Huyu hapa Shiney msikilize akizungumzia mziki wake, familia, mtoto pamoja na Baba mtoto... Bonyeza  HAPA

Msanii Wa BongoFleva Kuja Mombasa Kufuata Huduma Za Producer Amz

Image
Msanii wa bongo fleva kwa jina Rich One ambaye alifanya vizuri saana na ngoma hatuna kitu aliyomshirikisha juma nature,ameelezea matamanio yake ya kusafiri hadi kenya kuutafuta mkono wa producer wa mombasa Amz Wa Leo ikiwa nia muhimu ni kutayarishiwa bonge moja la project. Kulingana na Rich One ni kwamba ameamua kufunga safari hiyo kufuata huduma za Amz baada ya kuskia mdundo wa ngoma ya Cannibal na Juma Nature ambayo ilimdatisha saana kwa sababu ya utofauti wake. "Naja na Nature tuje tugonge bonge la ngoma na Nature , nimeskia ile ngoma ya Cannibal na Nature amepiga beat kali saana" ...... Rich One anapania kufanya project hiyo na mkongwe Juma Nature na huenda wakafika mombasa mda wa kama wiki mbili zijazo.

Je, Chapatizo Ameacha Mziki?

Image
Track yake ya mwisho kuachia ilikua mwanzo mwa mwaka huu, ni track ambayo aliachia kimyakimya sana hata wapo wengi hawana habari ya kua aliachia wimbo kwa jina VIGUDIGUDI . Pengine ilikua ndio ishara ya kwamba amechoshwa na pandashuka za mziki ndio maana akaiachia tu hivihivi, tofauti kabisa na wimbo alioshirikishwa na Dee Bouwy-NIPE. Kando na kuonyesha kutokua na msukumo na kazi yake ya mziki, Chapatizo ameonyesha kujituma sana katika u,MC, uchekeshaji na hivi karibuni uigizaji. Ni ishara ambazo zimeweza kuzua minong'ono ya kwamba Chapatizo huenda akwa ameacha mziki na kujitosa katika kazi hizo zingine ambazo zimeonyesha kumkubali kwa haraka na kumfanya aendelee kuishi vizuri. ''Uingiziaji na uchekeshaji nilianza toka 2014 ila ilikua ni filamu fupifupi za comedy lakini kwa sasa nimefanya filamu moja kubwa na Ashiner Pictures , watayararishaji wa kipindi cha Almasi . Tumemaliza ku,shoot filamu moja na ya pili tutaanza hivi karibuni. Ni filamu ambayo siwezi ion...

NEW VIDEO: Zureya Feat Dogo Richy - WARIDI WANGU

Image
Vipaji vipo hapa pwani, na Zureya   ni mmoja kati ya waliojaaliwa na kipaji kikubwa. Akiwa amemshirikisha Dogo Richy, hii ni track ya kwanza ya aina ya salsa kuwahi kufanywa hapa pwani. Ni mkono wa P roducer Emmy Dee . Ni video iliyoandaliwa na Johnson Kyalo.  

Msanii Wa Kike Kutoka Mombasa Aliyejibu Wimbo Wa Alikiba-AJE

Image
Grace Mueni ndio jina lake la serikali, ila katika anga za muziki anajulikana kama Ngunash . Ni msanii chipuka ambaye ameanza kupata kile ambacho wasanii wengi chipuka hukipigania-Aiplay. Hii ni baada ya kuachia track kwa jina NAJA . Ni track yake ya kwanza kuachia rasmi. Japo alishawahi ku,record track mbili, moja na producer TK2 na nyengine na Producer Triple A/ Mo Town Reords hajawahi kuziachia kwani ni juzijuzi tu ndio alisajiliwa na Mtwapa Records ambayo iko chini ya uangalizi wa Producer Mswazi Mayuro na mkataba wao hauruhusu ngoma hizo za mbeleni kuachiwa. 'niliposkia AJE ya Alikiba nilihisi kana kwamba alikua ananiimbia mimi, ndio nikapata mskuma ya kujibu wimbo ule na kutengeneza track hii'' ... Ngunash amenieleza. Ni track ambayo ameijibu kw ubunifu na ameonyesha uwezo wake wa sauti na Producer wake, Mswazi Mayuro ameitendea haki track hii. Download / Listen  HERE or HERE

Hustla Jay Aeleza Iwapo HipHop Inalipa

Image
Msanii hustla jay amefunguka na kupinga maadai kuwa Hip hop conscious hailipi.kulingana na hustla jay ni kwamba Hip Hop iko na utajiri mkubwa saana haswa ukifuata nguzo zake.  Hustla Jay amesisitiza kuwa mziki wa Hip hop unahitaji akili ya ziada kuufanya maana unakariri hali halisia ya maisha ya mtaani kupitia ujumbe wa yale mambo haswa yanayofanyika kwenye jamii.Je ni jinsi gani unaweza kujipatitia kipato kupitia mziki wa hip hop? Kulingana na Jay ni kwamba nguzo za hip hop kama vile street fashion unaweza pata lectures mahali ukafunza,corporate shows pamoja na mauzo ya muziki kwenye mitandao,ujasiriamali kupitia hip hop pamoja na kujihusisha kwenye projects nyingi zinazoizunguka jamiii.  Huyu hapa Hustla Jay akiizungumzia hip hop pamoja na miradi yake ikiwemo mradi wake wa hip hop and justice aliyomshirikisha jaji mkuu mstaafu Willy Mutunga . Msikilize HAPA

Nyota Ndogo Atumiwa Katika Utapeli

Image
Kila mtu ako mbioni kujitosheleza.... Wengi wako mbioni kutafuta pesa za kujikimu na wengine pia wako mbioni kutafuta mapenzi angalau roho zao zitulie wafarijike. Katika kutafuta pesa, wapo wanaotafuta pesa kwa njia halali wengine haramu ili mradi tu mwisho wa siku pesa iingie mfukoni. Na wanaotafuta mapenzi nao vilevile wanatumia njia tofauti kupata watakacho. Ukizingatia ya kwamba siku hizi mambo mengi yanafanywa mitandaoni, basi ni wazi kwamba utapata wengi wanapata pesa kupitia mitandao na wapo wanaopata wapenzi kupitia mitandao. Uganda kuna ukurasa wa facebook ambao unadai kukutanisha wapenzi. Ukurasa huo umebandika picha ya Nyota Ndogo akiwa na bwanake na wakidai kwamba hao ndio waliwezesha na kufanikisha wawili hao kukutana hadi kuishia katika ndoa. Katika ukurasa huo wamedai ya kwamba Nyota Ndogo anaitwa Sarah na bwanake ambaye jina lake ni Neilsen amebandikwa jina la Raymond. Juhudi za Nyota Ndogo za kufikia wenye ukurasa huo kupitia nambari za simu zilizow...

Rikky Bekko Ataja Vigezo Vya Kutoboa Kimataifa

Image
Mtayarishaji wa video za mziki anayefanya vizuri kwa sasa Ricky Becko amewahimiza wasanii kuwekeza vilivyo katika kazi zao ili kuongeza thamani ya bidhaa wanayoingiza kwenye soko la muziki. Kulingana na Becko ni kwamba njia pekee ya kupenya kwenye ramani ya mziki wa kimataifa ni kutoa kazi ambazo zitakua na ushindani mkubwa katika soko la sasa la mziki ambalo limezidi kuwa gumu kila kukicha. Becko amesema kuwa wasanii wengi wanatosheka na mafanikio madogo na wanakosa malengo makubwa katika kazi wanayoifanya.   "I think wasanii wengi wako kwa comfort zone... they are comfortable with what they have achieved like. Kuna watu wameingia kwenye mziki kwa sababu ya kupata fame, wengine kupata madame so mtu akiwa famous akipata tudem tunamuita ita pale basi ametoshek'' Becko amesema ili msanii kufanya kazi na yeye kwanza lazma msanii awe na talanta, pili lazima wimbo wenyewe lazima uwe na ubora. " msanii akija na wimbo ambao hauko kwenye viwango...

Producer Khalid Kuwashtaki Waandalizi Wa Tuzo Za Mombasa Awards 2016

Image
Producer ambaye hafichi hisia zake kila wakati pale anapokerwa au kufurahishwa na jambo flani haswa katika tasnia ya burudani, Prodcuer Khalid ameandika barua wazi kwa waandalizi wa tuzo za Mombasa Awards 2016. Tuzo hizo zimevutia hisia mbalimbali baada ya kutangaza orodha ya nominnees kama vile wasanii wengine kutoa katika tuzo hizo, Odinare Bingwa akiwa mmoja wao na wengine kusema hawataki kuhusishwa na tuzo zozote. Leo kupitia ukurasa wake wa facebook, Khalid amejitokeza na kuandika ujumbe huu akiuelekeza kwa maandaaji wa tuzo za Mombasa Awards huku akipendekeza sheria kutiliwa maana hata kwa maandaji wengine wa tuzo ili tuzo hizo ziweze kunufaisha wasanii si waandaaji wa tuzo tu.... To Whom it may concern, ‪#‎ MOMBASA_AWARDS‬ kwa miaka mingi wasanii wa pwani wamekuwa wakibebwa kama magunia ilihali wenzao wa Nairobi au Bongo wakibebwa kama mayai.Tuzo nyingi zilizopita zimekuwa na tabia ya kuweka wasanii kwa list zao bila taarifa, ilihali mshindi ashajulikana. Wasa...

Susumila Na Dazlah Wazozania Dancers

Image
Ni wiki ambayo imekubwa na fununu za madai kuwa msanii Susumila amewachukua dancers kadhaa kutoka kwa kambi ya Chilemonde na kuwasajili katika lebo yake ya Mishemishe Music Empire. Inavyojulikana ni kwamba wasanii hawa wawili ni washkaji wa karibu kwa kipindi cha mda mrefu wakiwa wamefanya vizuri pamoja katika ushirikiano wa track zao mbili Bangereba Remix na Kidekide ambazo zimefanya vizuri saana.  Je imekuaje kuaje mpaka Susumila akavuna kwenye shamba la Dazlah na kumchukulia dancers wake? Je ni kipi kilichowafanya dancers wakahamia Mishemishe Music Empire. Kuna ugomvi wowote kati ya kambi hizi mbili ama jamaa wamevurugana? Hawa hapa Susumila na Dazlah wasikilize wakifunguka kuhusu mzozo huu.. Wasikilize  HAPA

Complete/Final List Of Mombasa Awards 2016 Nominees

Image
Orodha Ya ya kwanza ya wateuliwa wa vitengo 11 vya tuzo za MOMBASA AWARDS 2016 vya kwanza iliachiwa hapo juzi, siku ya Alhamisi na hapo jana orodha ya vitengo 10 vilivyokua vimesalia ikaachiwa. Hivyo basi, ifuatayo ndio orodha kamili ya vitengo vyote 21 vya tuzo hizo zilizopangwa kufanyika Julai 16. Female Model of the year 1.Tima 2.Ruthalia Michaels 3.Leah T. 4.Lynn cyssy 5.Killian Maureen 6.Marriah Jamal 7.Faith Mwendwa Male Model of the year 1.Abdhulmtwalib saggaf 2.Nilesh Jentain 3.Talal Van Rocco 4.Erick Omtere Best Music Band 1.Wasojali Band 2.Yakuza Band 3.D-Sent 4.Juu Kua Band 5.Mafioso 6.C-Side 254 Best Fashion House/Designer 1.Rich Gang Classic Wear 2.Hotwear 3.Pamba Africa 4.Photie De souza(OG) Best Upcoming Artist 1.Rovy  Dahoah 2.King Julian 3. Mswazi Masauti 4.Team ocean money 5.Dully melody. 6.Loorysign 7.Silver D 8.Bawazir Beybe Actor/Actress Of The Year 1.Lucky collins 2.Prince Ali Bin Kubo 3.Juma Shibe 4.Eric Omtere 5.Qutie Qulthu...

Huenda Producer Tee Akatiwa Mbaroni

Image
Mwaka wa 2013, studio aliyokua akifanyia kazi Producer Tee , Da'Face Music ilivamiwa na vifaa vyote vikaibiwa. Aliyekua akimiliki studio hio ni Zakumera Zaky. Kwa kua Tee ndiye aliyekua amekabidhiwa vifaa hivyo ilibidi waingie katika makubaliano na Zakumera ya kwamba Tee ndiye atakayelipa hasara hio ya vifaa vilivyoibiwa.  Kulingana na mdokezi wetu ni kwamba vifaa vilivyokua vimeibiwa vilikua na thamani ya zaidi ya kshs.400,000 lakini wakaamua kushukisha thamani na kumpa wepesi Tee kwa kumuambie alipe kshs.252,000 . Katika makubaliano yao, ambayo nilifanikiwa kuona copy yake ni kwamba walikubaliana ya kwmba Tee alikua atalipa kshs. 10,000 kila mwezi. Kulingana na mdokezi wetu, toka Tee na Zakumera waingie katika makubaliano hayo mwaka wa 2013, Producer Tee amelipa kshs. 26,000 jambo ambalo limemgadhabisha Zakumera . Siku ya Jumatano, Producer Tee aliitwa katika kituo cha polisi cha Bamburi na kupewa amri ya kwamba alipe deni hilo alilonalo kufikia...

Mombasa Awards 2016 Nomination List

Image
Tuzo za Mombasa Awards 2016 zimepangwa kufanyika siku ya 16 mwezi wa Julai. Ikiwa leo ndio siku ya kutangaza wateuliwa wa vitengo mbali mbali wa tuzo hizo, hii hapa ni orodha ya kwanza ya ya vitengo 11 ambayo imeachiwa... Kulingana na waandalizi wa tuzo hizo Orodha ya vitengo vilivyobaki inatarajiwa kuachiwa baadae hii leo.. Best Male Artist 1.Susumila 2.Dazlah 3.Otile Brown 4.Sudi boy 5.Brown Mauzo 6.Amoury beybey Best Female Artist 1. Sis P 2. Serah sarah 3. Julliet Jovial 4.Akothee 5.Vivonce Wandia Best Dance Crew 1.Tsunami 2.Dabz All stars 3.Toxic Dancers 4.Jeke Jeke 5.G cleff 6.Mullaz 7.Exodus Movers Best Deejay 1.Dj Bones 2. Dj Phauz 3. Dj Ivory 4.Dj Electrick 5. Dj chris 6.Dj sashy 7.Dj skills Best MC 1.Mc Fortune 2.Mc Tucker 3.Mc Allano 4. Gates Mgenge 5.Mc Mike 6.Mc Lenium Blogger Of The Year 1.Machampali 2. Lil Guy G 3. Jackson Mulley 4. Godwin Pwani usanii 5. Backstreet Entertainment 6. Freddy Madebe Best Univesity 1.Techinical University of Mombasa(T.U.M) 2.Kenyatta Un...

Msanii Lil Mizze Kuhamisha Kambi Kutoka Malindi Hadi Mombasa

Image
Msanii kutoka maliandi ambaye track yake iliyopo hewani kwa sasa ni SIJUI KWANINI amefunguka ya kwamba anahamisha kambi yake hadi mjini Mombasa. Lil Mizze a mbaye anatarajia kuachia video ya SIJUI KWANINI mapema mwezi ujao amesema ya kwamba anapata ugumu kufanya mziki akiwa mjini Malindi. Mizze anasema changamoto anazozipata kwa sana zinasababishwa na yeye kua mjini Malinidi hivyo basi kuja Mombasa kutampa wepesi wa kazi yake ya mziki. 'Vitu vingi ninavyovihitaji ili kufanikisha mziki wangu vipo Mombasa, kama vile studio, vituo vya habari, ma,dj...so naona itakua vyema nikijisongeza karibu na resources hizi ili niweze kufanikisha safari hii yangu ya mziki." Lil Mizze amefunguka.

NEW MUSIC: Jay Madini- NYOTA YANGU

Image
Jay Madini ni msanii kutoka Mombasa ambaye yuko chini ya management ya MainSwitch iliyopo Nairobi. Kando na kuwa katika management, Jay ana manager binafsi kwa jina Morris Mbetsa . Aliachia track yake ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana kwa jina MY BABY na hii ni yake ya pili ikiwa inaitwa NYOTA YANGU. Ni track ambayo imesimama vizuri, si utunzi, si sauti, hata producer ameitendea haki track hii. Kati ya track nzuri zinazovutia hisia huu mwaka hii hapa ni moja yao. Download / Listen  HERE or  HERE

Wangenishirikisha, Yoyoba Remix Ingekua Kubwa- Producer Totti

Image
Hisia mseto zinazidi kuibuka kuhusu remix ya Yoyobah Remix ya Dogo Richie na Calvo Mistari ambayo ilitoka juzi.Track hii ilizua gumzo katika mtandao na kauli mpya kwa sasa inatoka kwa producer wa yoyobah original Producer Totti ambaye ameweka wazi mt azamo wake kuhusu track hiyo. ile copy yangu ndio ingekua remix kwa kua ndio ina nguvu zaidi, heri hii remix ndio ingekua origininal alafu ile yangu iwe remix kwa kua hii mpya imenimalizia idea yangu... Totti amefunguka .   Kulingana na Totti ni kwamba ngoma hiyo haijafikia hata kidogo viwango vya original track ambayo yeye ndio aliifanya... " Mimi kwa upande wangu ninapofanya kazi natamani ile kazi iwe kubwa,hakuna mtu anayetaka kujihusisha katika jambo ambalo halina maendeleo sababu nilikua nategemea ile remix itakua kubwa coz ingekua kubwa ningefaidika,dogo angefaidika na hao pia wangefaidika lakini kazi ikienda ifike mahali iwe haisongi tunakua tumeanguka sote,so mimi pia nimelaumiwa nimepigiwa simu na w...

Kibibi Salim Aongelea Uigizaji Na ndoa Yake

Image
Msanii wa filamu Kibibi Salim anayebeba uhusika wa ''chiriku' ' kwenye tamthilia ya Almasi amefunguka na kuwahakikishia wote walio na ndoto ya kuingia katika tasnia ya uigizaji kuwa tasnia hiyo ya uigizaji iko na hela ila kinachohitajika ni talanta, bid ii na subira. ''ukiona nimetulia silalamiki kwenye hii sanaa ya uigizaji jua naridhika na ninachokipata. Sanaa ya uigizaji inalipa, nime,settle hapo  kwa sababu inalipa hata kama atfiirst haitakulipa inavyotaka ila mtu huanzia chini..'' Kibibi ameeleza. Kibibi ambaye pia ni mke wa ndoa wa msanii Susumila amesema kuwa yuko mbioni kupitia msaada wa mumewe kufungua studio yake itakayoshuhulika na utayarishaji wa filamu miaka miwili ijayo. Mbali na mipango yake kwenye uigizaji, Kibibi pia amefunguka mengi na MtuBei kuhusu ndoa yake na msanii Susumila. .kwa kina zaidi fuata link kumsikiliza Kibibi kwenye mahojiano na MtuBei HAPA

NEW MUSIC: Yamoto Band Feat Ruby - SUU

Image
Huu mwaka wamepunguza kazi sana ukilinganisha na mwaka jana ambapo walikua wanatoa track baada ya track. Band inayotamba sana Afrika Mashariki, Yamoto Band (Mkubwa Na Wanawe) wamevunja ukimya wao na track hii ambayo wamemshirikisha mrembo mkali wa sauti, hitmaker wa Forever, Ruby. Ni track ambayo imeandaliwa na Producer wa Mkubwa Na Wanawe, producer mkali sana kutoka pwani ya Kenya ( Mombasa), Producer Shirko. Download / Listen  HERE

Wasojali Band & Kelechi Africana- NITALIA NAWE ( Extended Version)

Image
Hii hapa ni extended version ya video ya track ya Wasojali Band na Kelechi Africana ya video yao ya Nitalia Nawe. Ni version ambayo imetayarishwa na Beat Link .

Dogo Richy Awajibu Wanaoiponda Yoyoba Remix

Image
Msanii Dogo Ree tokea juzi amekua akigonga vichwa vya habari baada ya kuachilia video ya Yoyobah Remix aliyomshirikisha Calvo Mistari . Baada tu ya Richie kuachilia video hiyo baadhi ya washikadau pamoja na mashabiki wa mziki walivamia mta ndao na kuiponda video hiyo huku wengi wakidai kuwa ni mbovu na haijaipiku Yoyoba original. Baada ya mitazamo kibao kuanikwa kwenye mitandao, Richi e amefunguka na kuweka wazi kuwa anaheshima maoni ya kila mtu..... "Mimi ninaheshimu maoni ya kila mtu ila wangeisifu yoyobah original kiwango cha vile wanavyoiponda remix then ningefika mbali saana,alafu mimi ningewasihi watu kuwa hakujaharibika kitu sababu kama remix haujaipenda original ipo unaweza ipa shavu" Huyu hapa Dogo Richie msikilize ujue anaowatupia lawama pamoja na mtazamo wake kuhusu remix hiyo...Je yeye mwenyewe ameikubali ameikubali? Bonyeza  HAPA

Gates Mgenge Aongelea Kuhusu Kuhongwa Na Wasanii

Image
Mtangazaji maarufu wa kituo cha PiliPili Fm, Gates Mgenge amejitenga na lawama ambazo kwa kipindi cha mda mrefu zimemuandama kuwa amekuwa akipendelea wasanii flani katika kipindi chake. Kulingana na Gates ni kwamba hawezi kamwe kumpendelea wala kubana mziki wa msanii yoyote. "cha msingi na sekondari mi kazi huingia saa tano mpaka saa moja na huwa napata kila kitu kishapangwa mziki ushapangwa na nikaambiwa link zangu ni ngapi so cha msingi kwangu ni sauti na creativity yangu lakini maswala ya mziki gani nitakaocheza hapo ni pagumu maana hiyo ni kazi ya ma producer wangu"..... . Gates ambaye pia ni MC maarufu katika mkoa wa pwani pia amekana madai kuwa huwa yeye amependelea wasanii flani katika shows zinazoandaliwa huku akisema kuwa hajawahi husika kabisa kwenye kuchagua wasanii kutumbuiza kwenye shows. Huyu hapa Gates Mgenge , akieleza vigezo halisi vinavyohitajika ili mziki wa msanii upitishwe na ma producer wa show yake pamoja na siri ya kutawala shows za pwan...