Donde Samora Ajitosa Kwenye Siasa
Ni mtangazaji wa redio mkongwe hapa mkoani. Alianza kupata umaarufu mwaka wa 2000 alipojiunga na Baraka FM. Mwaka wa 2004 alijiunga na Pwani FM , kituo cha redio kinachomilikiwa na Shirikika La Utangazaji Kenya(KBC) hio ilikua ni kabla ya kujiunga na Pilipili FM Mwaka wa 2013. Ikiwa ni mda ambao watu wanajitayarisha na uchaguzi wa mwakani, watu wengi wameonyesha azma yao ya kuwania vyeo mbalimbali katika uchaguzi ujao. Donde naye hajaachwa nyuma kwani hapo jana, Jumapili ya 28 Februari, akihudhuria misa katika kanisa la katoliki Juda , Donde alitangaza rasmi ya kwamba anajitosa katika ulingo wa kisiasa na anapania kupigania kiti cha MCA , wodi ya Junda. Donde alisistiza ya kwamba maamuzi yapo mikononi kwa wananchi ya ni wajibu wa kila mwananchi ahakikishe ya kwamba amejisajili kama mpige kura ili ifikapo katika uchaguzi awe na uwezo wa kufanya maamuzi kwa kuchagua viongozi wanaostahili.