Hii leo katika Kipindi cha MwakeMwake , kinachoendeshwa na Gates Mgenge, Pilipili Fm , kuanzia saa tisa jioni hadi saa moja usiku Susumila amefunguka ya kwamba ana jumla ya pete kumi na tano na kati ya pete hizo, ile ambayo ina thamani zaidi ni ya gharama ya .... Je pete zote hizi ni za nini? Kwa mda mrefu saana sintofahamu imegubika kitendo cha msanii Susumila kumiliki na kuvaa pete kibao sana mikononi mwake huku baadhi ya watu wakifikia kiwango hata cha kuhusisha pete hizo na nguvu za giza. Kwa mara nyingine Gates ametaka kufafanuliwa zaidi umuhimu wa pete hizi kwa maisha ya Susumila. Nikimnukuu Gates .."labda pete zako huwa wazitumia na nini, ni mapambo au maanake one time Chapatizo alisema kwamba hapa Mombasa na huu mziki hauwezi fanya bila kujikinga".. swali hili Susumila akalijibu, nikimnukuu "kila mtu huwa anafanya vitu apendavyo yeye mwenyewe, kuna mwingine anafuga rasta kwa sababu ya dini yake, wengine wanafuga rasta kwa kuwa ni fashion, umenielew...